Showing 41–60 of 112 results

Kaputula la Marx

KShs590.00
Kaputula la Marx ni tamthiliya pekee ya Euphrase kezilahabi.

Mtafiti by Hussein Issa Tuwa

KShs990.00
Habari ya kuuawa kwa mtafiti Grayson Mochiwa haikuwa na sababu ya kumshitua mrembo Zay mpaka pale anapogundua kuwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa rafiki yake kipenzi sio tu hakukuwa kwa bahati mbaya bali pia kulihusiana moja kwa moja na kifo kile kibaya cha mtafiti Grayson Mochiwa.

Nyerere na Vijiji vya Ujamaa

KShs590.00
Msingi na dafina ya tamthilia hii ni historia na lengo kuu la Mwalimu Julius Nyerere na TANU kutaka kujenga uchumi wa ujamaa na kujitegema mintarafu mwongozo wa kitabu cha azimio la Arusha, 1987.

Nagona

KShs690.00
Nagona ni riwaya fupi ya kifalsafa na kibaadausasa inayoibua fikira kuhusu falsafa na maana ya uhai, maisha, dhamira na hata fikira yenyewe.

Dunia Uwanja wa Fujo

KShs1,090.00
Dunia Uwanja wa Fujo ni riwaya inayohusu mgongano wa kimfumo na kitabaka kati ya ujamaa n aubepari kwenye miaka ya 1960 na 1970 nchini Tanzania.

Usiku Utakapokwisha by Mbuda Msokile

KShs590.00

"Usiku Utakapokwisha" ni riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Mbunda Msokile inayochunguza changamoto za kijamii na kiuchumi zinazowakumba vijana nchini Tanzania, hususan matatizo ya ukosefu wa ajira. Hadithi inawafuata vijana watatu — Chioko, Gonza, na Nelli — wanaojitahidi kufanikisha malengo yao ya maisha licha ya vikwazo hivi.

Gonza, akiwa amechoshwa na tofauti kati ya ugumu wa maisha yake na urahisi anaouona kwa wengine, anaamua kutafuta njia ya mkato ili kufanikisha ndoto zake. Kwa upande mwingine, Chioko anawakilisha mtazamo wa subira na uvumilivu, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kupambana. Riwaya inafuatilia matokeo ya maamuzi ya Gonza na kuuliza swali kuu: Ni lini usiku wa matatizo utaisha?

Kazi hii ya fasihi inangazia kwa kina mada za umasikini, ukosefu wa fursa, na athari za ukosefu wa haki za kijamii kwa mtu binafsi na ndoto zake.

Mkwe wa Jaji Mkuu by Wilbard Makene

KShs990.00
Jaji Mkuu Athumani anapata taarifa kuwa bintiye Huruma ana mahusiano ya kimapenzi na Mayunga, mtoto wa mfanyabiashara mkubwa. Mtaani, tetesi zimezagaa kwamba Mayunga ana mahusiano na watuhumiwa wa dawa za kulevya. Athumani hapendezwi. Anatofautiana na Huruma. Inambidi Mayunga ajisafishe huku akihatarisha maisha yake.

Shujaa Mirambo by Emmauel Mbogo

KShs690.00
Tamthilia hii ya kihistoria inamhusu Mirambo.

Mkono Wa Jamhuri by Wilbard Makene

KShs990.00
Kabrasha la Rais ni riwaya yenye kusisimua iliyosheheni visa na mikasa: visasi, mapenzi na usaliti.

Kabrasha La Rais by Wilbard Makene

KShs800.00
Kabrasha la Rais ni riwaya yenye kusisimua iliyosheheni visa na mikasa: visasi, mapenzi na usaliti.