Showing 1–20 of 32 results

Aliyeonja Pepo: Tamthilia by Farouk T...

KShs590.00
Juma Hamisi, Muislam safi kutoka Bagamoyo anafariki, na roho yake inaenda Mbinguni. Baadaye inafahamika kuwa hili ni kosa kubwa lililofanywa na Ziraili, Malaika mtoa roho. John Houghton wa Uingereza ndiye aliyestahili kutolewa roho siku hiyo. Ili kutatua tatizo hili, roho ya Juma Hamisi inabidi irudishwe duniani. Baada ya majadiliano ya muda na ili kuficha kosa hili lisigunduliwe, Ziraili na wenzake wanakubaliana kuirudisha roho ya Juma katika mwili mwingine, hata kama ni mwili wa paka.

Uchungu wa Mwana na Hadithi Nyingine

KShs1,400.00 KShs1,000.00
Baina ya siku ya kuzaliwa na ya mauti, binadamu hukumbana na kukabiliana na pandashuka kemkem. Bi. Safari anajua hili fika. Maisha yake yamemwonjesha asali na shubiri kwa wakati mmoja. Analazimishwa ndoa na baba yake aliyemkuza katika maisha ya fimbo mkononi. Kisha ndoa inaingia doa anapokosa kuhimili. Anapovumilia na saburi yake kulipa, anapata mwana kisha dunia inamchukua mtoto wake wa pekee. Ni pigo linalohitaji moyo wa jiwe kustahimili. UCHUNGU WA MWANA na Hadithi Nyingine ni antholojia iliyofum-wa kwa miyaa ya lugha ashirafu na nyuzi za misamiati ya kuhusudi-wa. Imeyamulika waa maisha ya sasa na kuyaweka peupe ya jana na kesho. Visa vyote vimeshiba fani aula na aali zitakazomfanya msomaji kutokinai kwa haraka. Imejumuisha waandishi wenye ukwasi na ustadi kamili wa lugha na wanaoelewa masuala mtambuko na yanayoibuka katika maisha ya sasa. Inajivunia anwani zenye mvuto na maudhui yenye utajiri mkubwa wa lugha na mafunzo. Diwani hii inafunza, inaadibu, inaadili, inaonya na kutahadharisha jamii dhidi ya tamaa, ubinafsi na mambo hasi yanayoikwaza jamii husika. Wahariri wake wameivalia njuga na kuihakiki kwa makini ili kupakulia wasomaji uhondo wa fasihi isiyowekeka chini. Ustadh Kamau na Kaka Fred ni mfano aula wa wahariri mahiri wa fasihi.

Kitumbua Cha Mauti na hadithi nyingine

KShs1,300.00 KShs1,000.00
Katika pilkapilka za kulivuka daraja la ukata ili kuupakata ukwasi, wapo wa-tumiao njia mkato na wapo wajitumao kwa bidii na haki wakimaizi kuwa hawafai kuwa kupe. Kitumbua cha mauti ni antholojia iliyosukwa ikasuki-ka kama mswala. Imejumuisha waandishi wenye utaalamu wa hali ya juu na wenye macho mapevu yaliyoangaza maudhui ya kisasa. Inajivunia anwani anuai zenye mafunzo ya heki-ma na tabasuri zinazotahadharisha na kueneza injili ya usawa na kupinga mitazamo hasi katika jamii ya wanaleo. Wahariri wamepiga mbizi na kuzuka na upanzi muafaka utakaokufanya ukienzi Kiswahili na fasihi. Kaka Fred, Ustadh Kamau na Okwalo Wambani ni mfano tosha wa wahariri mahiri wa fasihi. Visa vina tamathali aali aali zitakazomfanya msomi kutoiweka chini nakala hii. Ama kweli hutahema na kushika tama kwa kujinyakulia diwani hii. Usingoje kuhadithiwa jamani! Kaa mkao wa kula ule shibe yako.

VIRUSI by MUTWIRI MARETE

KShs967.00 KShs580.00

‎Virusi vimezuka kutoka taifa la Mashariki na kuutikisa ulimwengu. Kama ilivyo katika mataifa mengine, wananchi wa Ukaragosi wanakumbana na hatihati kukabiliana na mabadiliko yanayotokana na msambao wa virusi hivyo. ‎ ‎Wapo wananchi kama vile Validus ambao, licha ya hatari ya Virusi vya Uviko, anaamini kuwa Ukaragosi kuna Virusi hatari zaidi kuliko Uviko. ‎ ‎Je, kuna virusi vipi vingine hatari Ukaragosi? Tamthilia ya Virusi inamchorea msomaji taswira ya matukio yanayoathiri mataifa mengi hasa yale yanayostawi.

Sikitiko la Heri by Mufti Moulid

KShs450.00
Sikitiko la Heri ni tamthilia la kifeministi. Upekee wake mkubwa unatokana na jinsi mwandishi anavyotumia lugha kwa urahisi lakini kwa jazanda kubwa.

Mwongozo wa Bembea ya Maisha by John ...

KShs450.00 KShs380.00
Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kumrahisishia mwalimu na mwanafunzi kazi na kumpa mwelekeo unaofaa. Kitabu hiki kimeangazia masuala ibuka katika utahini wa karatasi ya tatu ya Kiswahili katika mtihani wa KCSE. Kitabu hiki kimejumuisha vipengele saba vya uhakiki wa fasihi andishi kama vile; Ploti ya tamthilia, dhamira ya mwandishi, mandhari na umuhimu wake, ufaafu wa anwani, maudhui, wahusika na uhusika na mbinu za lugha. Maswali ya udurusu pia yamejumuisha katika kila mwisho wa onyesho ambayo yatamsaidia mwanafunzi kujinoa na kujipima ratili uelewa wake wa ploti. Maswali ya kiwango cha kitaifa pia yamejumuisha pamoja na majibu yake. Masuala ibuka kama vile umuhimu wa wahusika, mbinu za kimtindo, aina za takriri, aina za taswira, na vipengele vingine.