Showing all 13 results

Kumng’oa Nduli na Emmanuel Mbogo

KShs590.00
Tamthiliya hii inaakisi awamu mbili za utawala wa Diktera Idi Amin nchini Uganda Awamu ya kwanza ni kuanzia mwaka 1971 alipomng'oa Milton Obote na kujitangaza Rais wa maisha wa nchi ya Uganda. Katika awamu hii, mwandishi anasawiri utawala wa kikatili, mateso, vifungo na hata mauaji ya raia wa madaraja yote katika jamii. Awamu ya pili, Oktoba, mwaka 1978, jeshi la Idi Amin lilivamia Mkoa wa Kagera, nchini Tanzania. Katika uvamizi huu, wanajeshi wa Uganda walimuua Hans Poppe, Mkuu wa Polisi na raia wengine wengi na kutangaza kuwa Mkoa wa Kagera ulikuwa sehemu ya Uganda. Shambulio hili linasababisha Mwalimu Julius Nyerere kutangaza vita dhidi ya Nduli kupitia ile hotuba maarufu, akisema: Wamanchi! Sasa tuna kazi maja ta! Кumpiga! Sahabu ya kampiga tunaya! Niya ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga tunayo! Mwandishi anaonesha kuwa, hatimaye, mwaka 1979 Nduli Idi Amin aling'olewa na wanajeshi wa JWT. Akakimbilia Libya, na kufariki dunia akiwa huko Saudi Arabia, tarehe 16/8/2003. Hii ni tamthiliya muhimu kwa kila mpenda amani, haki na maendeleo kote duniani.

Kaputula la Marx

KShs590.00
Kaputula la Marx ni tamthiliya pekee ya Euphrase kezilahabi.