Showing 21–40 of 112 results

Dhifa by Euphrase Kezilahabi

KShs590.00
Dhifa ni diwani ya mwisho ya Kezilahabi. Diwani hii inakusanya tungo za miaka ya 1990-2008, wakati wa mageuzi ya kiliberali mamboleo yaliyoasisiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi na kuendelezwa na warithi wake baada ya Mwalimu J.K. Nyerere kustaafu. Jina la diwani linaakisi wazo lake kuu: "Dhifa" - yaani sherehe ya kujinufaisha baada ubinafsishaji na uporaji wa mali na rasilimali za Umma. Jina la diwani hii linabeba motifu kuu ya kipindi hicho: ufisadi na ubadhirifu uliokithiri.

Malenga Wa Bara by Mulokozi and Kahigi

KShs890.00

Mwanzoni mwa miaka ya 1970 palitokea mgogoro wa ushairi katika nchi za Tanzania na Kenya. Makundi mawili, yaliyoitwa "wanamapokeo" na "wanausasa", yalibishana kwenye magazeti, vitabuni na kwenye makongamano kuhusu maana na maumbo ya ushairi. Miongoni mwa matokeo mazuri ya mgogoro huo ni kuandikwa na kuchapishwa kwa makala mengi na vitabu kadha vya nadharia na mikusanyo ya ushairi. Diwani ya Malenga wa Bara ni tunda mojawapo la mgogoro huo. Watunzi wa mashairi yaliyomo humu, K.K. Kahigi na M.M. Mulokozi, walikuwa miongoni mwa waanzilishi na washiriki wakubwa wa mgogoro huo. Hivyo mashairi yao yenye maumbo na miundo mbalimbali ya "kimapokeo" na ya "kisasa", ni kielezo cha kivitendo cha nadharia yao ya ushairi. Aidha, mashairi haya yanaakisi vizuri vuguvugu na mikikimikiki ya kisanaa, kijamii na kiitikadi ya miaka hiyo ya 1970.

Moto wa Mianzi by M.M Mulokozi

KShs690.00
Riwaya ya Moto wa Mianzi inahusu matukio yaliofuatia kutekwa kwa ngome ya Kalenga mwaka 1894.

Julius Nyerere Kizimbani by Emmanuel ...

KShs590.00
Tamthilia hii inahusu tukio la kweli la kihistoria lililotokea mwaka 1985.

Mwinyi na manyani ya adili by Emmanue...

KShs690.00
Tamthilia hii inazungumzia hali ya maisha nchini Tanzania kabla na wakati wa utawala wa rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi(Mhe).

Nguzo Mama by Penina Muhando

KShs590.00
Nguzo mama ni tamthiliya inayozungumzia changamoto zinazowakabili wanawake kwenye jamii ambazo zimekuwa minyororo inayowazuia kufikia kilele cha ukombozi wao.

Nyerere na Safari ya Kanaani by Emman...

KShs690.00
Msingi na dafina ya tamthilia hii ni historia na lengo kuu la Mwalimu Julius Nyerere na TANU kutaka kujenga uchumi wa ujamaa na kujitegema mintarafu mwongozo wa kitabu cha azimio la Arusha, 1987.

Operesheni Chakaza: Masimulizi ya Vit...

KShs890.00
Huwezi kuelezea historia ya taifa ya Tanzania bila kugusia vita vilivyotokea mwaka 1978-79 kati ya Tanzania na Uganda. Hata hivyo , yapo  maswali mengi ya kujiuliza. Nini kilimfanya Idi Amin avamie Tanzania? Ni vikwazo gani wanajeshi wa Tanzania walikabiliana navyo kwenye medani ya vita? Silaha gani zilizotumika? Siri ya ushindi wa Tanzania ilikuwa nini? Kwanini Uganda ilishindwa? Kapteni Mulokizi anatoa majibu ya maswali haya pamoja na mengine katika kiabu hiki muhimu kwa ajili ya kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Kumng’oa Nduli na Emmanuel Mbogo

KShs590.00
Tamthiliya hii inaakisi awamu mbili za utawala wa Diktera Idi Amin nchini Uganda Awamu ya kwanza ni kuanzia mwaka 1971 alipomng'oa Milton Obote na kujitangaza Rais wa maisha wa nchi ya Uganda. Katika awamu hii, mwandishi anasawiri utawala wa kikatili, mateso, vifungo na hata mauaji ya raia wa madaraja yote katika jamii. Awamu ya pili, Oktoba, mwaka 1978, jeshi la Idi Amin lilivamia Mkoa wa Kagera, nchini Tanzania. Katika uvamizi huu, wanajeshi wa Uganda walimuua Hans Poppe, Mkuu wa Polisi na raia wengine wengi na kutangaza kuwa Mkoa wa Kagera ulikuwa sehemu ya Uganda. Shambulio hili linasababisha Mwalimu Julius Nyerere kutangaza vita dhidi ya Nduli kupitia ile hotuba maarufu, akisema: Wamanchi! Sasa tuna kazi maja ta! Кumpiga! Sahabu ya kampiga tunaya! Niya ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga tunayo! Mwandishi anaonesha kuwa, hatimaye, mwaka 1979 Nduli Idi Amin aling'olewa na wanajeshi wa JWT. Akakimbilia Libya, na kufariki dunia akiwa huko Saudi Arabia, tarehe 16/8/2003. Hii ni tamthiliya muhimu kwa kila mpenda amani, haki na maendeleo kote duniani.