Showing 1–20 of 116 results

KAGA by Janet Opiyo

KShs700.00
Novela ya Kaga inaangazia msichana Saida Jitihada ambaye anafikwa na mengi maishani. Hayati baba yake mzazi, Bwana Sanifu Jitihada , mwalimu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili anagonga vichwa vya habari kwa usanifu na ubunifu wake. Saida anampoteza mama yake siku ya kutangazwa matokeo yake katika mtihani wa kitaifa. Binti Jitihada anajitoma katika huba na Siti Mlungwi, mjukuu wake Bwana Hasidi. Hasidi mkubwa wa aila ya Jitihada. Je, Saida ataweza kukabiliana na changamoto hizi na kusimama imara dhidi ya upinzani unaoikumba familia yake?

Mwanzo wa Mwisho na Mwarabu Omari Mwa...

KShs449.00 KShs399.00
Kwikwi za vilio vya bi harusi zinasikika kwa mbali. Kalazimishwa kuwa mke wa mtu, ndoto yake imevunjwa na kusagwasagwa bila ya huruma. Kavalishwa gauni la kiyombo, kichwani katundikwa taji la leso lililopachikwa viwangwa vinavyong`aa. Machozi yanamtoka machoni na kuuharibu wanja aliopakwa. Naam machozi. Si machozi ya furaha bali ya karaha. Binti wa miaka kumi na mitatu hatimaye anaenda kufunga ndoa na mzee wa miaka tisini. Je huu ni mwisho wa ndoto yake Bi harusi aliyoiwekeza toka angali kinda? Ama ndio mwanzo wa shida zake kuisha? Mwanzo wa Mwisho ni riwaya iliyojikita nchini Fokota. Wanawake wa jamii hii wametengwa na kudharaulika. Wao hawana kauli mbele ya wanaume. Mateso, binti aliyekulia kwenye utandabui wa unyanyapaa alijikusuru kuing`oa mizizi hiyo. Je atakumbana na yepi njiani? Na je atafaulu? Mwarabu Omari Mwarabu ni mwandishi anayechipuka kwa kasi mno kwenye sanaa ya utunzi wa hadithi za kiswahili. Alizaliwa Bodo, Kaunti ya Kwale mwaka wa 2000. Mwanzo wa Mwisho ni riwaya yake ya pili baada ya ile ya kwanza iitwayo Daraja la Mauti. Kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo , anasomea Shahada ya Takwimu na Tarakilishi. Pia ni mwanachama wa CHAWAKAMA Kenya.

Usiku Mmoja by Bahati Miti

KShs400.00
Usiku Mmoja ni riwaya ya kusisimua inayofumbua uhalisia wa maisha ya mjini yanayohusisha vijana, wanasiasa na wafanyabiashara wenye nguvu. Lugha iliyotumika ni ya kusisimua; na kinanuia kutoa tahadhari na kuelimisha jamii, hasa vijana kuhusu umuhimu wa kufanya maamuzi mazuri

NIZIKWE KWETU KIAMBONI by BENSON MUGO

KShs700.00

Nizikwe Kwetu Kiamboni ni riwaya inayochambua na kufafanua kwa undani madhila yanayoikumba nchi ya Kafila inayoongozwa na kiongozi aliye na uroho wa kutwaa mali yote ya nchi hiyo.

Tufani Ya Maisha by Boniface Limiri

KShs1,200.00 KShs1,000.00
Baada ya dhoruba, kuna utulivu… baada ya machozi, kuna tabasamu.” Hii ni hadithi ya familia inayopambana na mapito ya maisha ndoto zikivunjika, ndoa ikitikisika na matumaini yakizimika lakini bado upendo na imani vinapigania nafasi ya pili. Ni simulizi ya kugusa moyo, iliyojaa mafunzo ya maisha, msamaha, mshikamano na tumaini jipya. Kila kurasa inakuuliza: una nguvu ya kusamehe? Una imani ya kusimama tena baada ya kuanguka? Kitabu hiki si hadithi tu ni mwaliko wa kugundua mwanga katikati ya giza. Je, Ladama ataweza kusimama imara mbele ya tufani za maisha? Je, upendo wake kwa Sadia utamwokoa, au utamwan-gusha? Na je, ataweza kuchagua msamaha badala ya chuki au ataangamia katika kivuli cha maamuzi yake?

Maisha ya Mwanaharamu by BENSON MUGO

KShs550.00
Maisha ya Mwanaharamu ni riwaya inayosimulia kisa cha kijana mmoja anayezaliwa nje ya ndoa. Hii ni kulingana na mtazamo wa wanakijiji cha Deka. Kijana huyu anachukuliwa kama mlaanifu na anachukiwa na takribani kila mja katika kijiji hiki. Madhila anayoyapitia yanasababisha afe moyo hivi kwamba anaamua kujitia kitanzi katika Msitu wa Aguzi lakini Ibra, Mungu wa Kijiji cha Deka, anayaokoa maisha yake.

Adhabu Ya Maisha By Elishaphan Wachira

KShs500.00 KShs449.00
Mwaisambe alipata taarifa kwamba katika jimbo lao la Matusitusi kulikuwako na mganga mashuhuri. Mganga huyo aliwatibu watu kwa dawa za kienyeji alizokuwa nazo daima. Basi baada ya kusikia habari kumhusu mganga huyo, Mwaisambe aliamua kwenda kumtembelea. Ndugu Mwaisambe anaonekana kuishi maisha ya kubahatisha. Ni mfano wa vijana wanaoonekana kukosa ruwaza, wanabebwa hobelahobela na upepo wa nakama na kuwaangamiza. Mwaisambe yu safarini kumtafuta mganga mashuhuri asiyemjua asili wala fasili yake. Anapanda milima na kuivuka miamba hadi katika eneo la Kivunja Kimya. Atafaulu kumpata mganga wake? Jisomee upate kujua… * Bwana Elishaphan Wachira ni miongoni mwa waandishi wanaochipuka kwa kasi sana. Anajikusuru daima kuandika kwa lugha ya Kiswahili na kukiendeleza. Kwa sasa ni mwalimu wa Kiswahili katika shule ya upili ya Wasichana ya Rarakwa katika Gatuzi la Murang’a. Anajaribu kwa udi na uvumba kukiendeleza Kiswahili kupitia kazi bunilizi. Kwa sasa anamiliki shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kengeza La Jasiri By Shisia Wasilwa

KShs749.00 KShs699.00
Jasiri ana Kengeza. Kengeza hilo halimpi amani. Linamsumbua maishani. Hilo kengeza linayaunganisha maisha yake ya zamani na usasa. Kalipata ujanani. Amekataa kulizika katika kaburi la sahau. Je, Jasiri atapata tiba ya kengeza hilo analopenda, kulificha pembeni mwa kijoyo chake? Anagundua pia marehemu babake kaaga dunia kutokana na hilo kengeza. Je, haya makengeza ndiyo nini? Ni masimulizi yanayonata, yaliyosheheni taharuki na maudhui mazito. Kuhusu mwandishi Shisia Wasilwa ni mwandishi na mwanahabari stadi wa siku nyingi. Aliwahi kuhudumu na Shirika la Habari nchini Kenya-KBC, China Radio Kimataifa, Citizen Tv na Radio, BBC na Deutsche Welle-DW. Baadhi ya kazi zake ni pamoja Makovu ya Uhai na Dunia Tambara Bovu. Alihariri Ndoto ya Almasi chake Ken Walibora, mwongozo wa Utengano wa Said. A. Mohammed miongoni mwa kazi nyingine teule. Kwa sasa anazamia shahada ya uzamili katika masuala ya mawasiliano katika chuo Kikuu cha Aga Khan.

Nyumba Ya Msonge Ya Nyanya Yangu

KShs300.00 KShs230.00
Title: Nyumba ya Msonge ya Nyanya Yangu Series: Msururu wa Discovery Author: Toroitich Patrick Yegon Target Class: Early Readers grade 1-3 Hadithi hii inalenga kukuza uelewa wa watoto wa mazingira yao na kuwawezesha kutunga hadithi kuhusu vifaa, wanyama, maliasili na vitu vingine vingi wanoatumia kila siku. Hadithi hii imeandikwa kulingana na maisha ya kijijini. Inazungumza kuhusu maisha yake nyanya ya msimulizi na jinsi anavyoishi na wanajamii wengine, marafiki, wageni na pia wanyama wao.

Kichala cha Ushairi by Nickson Hamisi

KShs630.00 KShs599.00
Kichala cha Ushairi kimeshughulikia BAHARI na AINA zote za mashairi na pia kimeshughulikia maswali yote ya mitihani ya KITAIFA KCSE kwanzia mwaka 2007-2023 na mwongozo wake.

Likizo Mashambani by Toroitich Patric...

KShs500.00 KShs350.00
Title: Likizo Mashambani Series: Hadithi za Kiafrika Author: Toroitich Patrick Yegon Target Readers: Class 5,6,7,8 Hadithi hii inasimulia matukio aliyoyapitia Shani alipozuru kijijini Kaplelekwo wakati wa likizo ya Aprili. Katu Maishani Shani hakuwahi kutarajia kuwa angewahi lia kwa kuondoka Kaplelekwo kama alivyofanya siku hiyo alipokuwa akienda kuabiri gari lililokuwa likimngoja.

Mfalme Katili

KShs600.00
Mfalme Katili ni hadithi ya nguvu, usaliti, na ujasiri, ikichora mstari wa dhoruba ya hisia na mapambano ya ndani na ya nje—kitabu cha kutisha, kinachotia moyo, na kinachokumbusha kuwa haki haiwezi kuzimwa milele.

Maisha Pilipili

KShs450.00 KShs400.00
Maisha Pilipili ni novela inayoelezea uhalisia wa maisha. Mbona tamaa inamzingira binadamu?

THE ILLEGITIMATE MOTHER

KShs800.00
"Are you insane Mr. Governor? This is pure gold! Do you want to say we will bury gold? Six feet? I will not allow. Can't we hire Faruk to get us a good coffin from his workshop?..." The Illegitimate Mother is a fascinating story about a mother whose greed surpasses her love for her own family. A mother is akin to God. She is an epitome of love and care. However, the mother in this story is a mother who is an insult and a blot to motherhood. RUTERE SHENVER D. Is a teacher, a poet and the Author of the best selling book _*' The Beads of Doom'.*_ His other popular books include; _Ushanga, Ngalawa Gharikani, The Malik, The Beads of Doom, Two Pots of Witchcraft, The Cruise Nightmare, Imarisha Sarufi among others.