Showing 61–80 of 116 results

PESA WEWE! by FREDRICK OMINA

KShs1,500.00 KShs1,250.00
Fedha ni mtumishi mzuri lakini bwana mbaya. Zinapopewa nafasi ya kututawala, hutupotosha; lakini tunapozitawala kwa hekima, hutufungulia milango ya mafanikio na maendeleo. Hivyo basi, hata kama ulianguka jana, bado unaweza kusimama leo. Hata kama ulipoteza mengi, bado unaweza kujenga upya. Maadamu una pumzi, una nafasi ya kuanza tena.

Utubora Mkulima by Shaaban Robert

KShs790.00
Kitabu hiki kinasimulia maisha ya kijana Utubora, ambaye anapitia changamoto za maisha, mafanikio ya kimali, na hatimaye kuchagua kuishi maisha ya kilimo na kuridhisha nafsi yake kwa misingi ya ukweli na uadilifu.

Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam

KShs790.00
"tenzi za marudi mema"ni tafsiri na marekebisho ya kitabu cha mashairi ya kifalsafa ya mshairi maarufu wa Uajemi, Omar Khayyam, yaliyotafsiriwa na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili na mtunzi mahiri wa Afrika Mashariki, Shaaban Robert. Kitabu hiki kinazungumzia maana ya maisha, kupita kwa wakati, na busara ya kuishi kwa amani na matendo mema.

Sanaa ya Ushairi by Shaaban Robert

KShs790.00
Saana ya Ushairi ni mwongozo maalum unaofafanua dhana, misingi, na sheria za utunzi wa mashairi ya Kiswahili. Kinatoa mchango mkubwa katika kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa mashairi ya jadi yenye ufasaha na maadili.

Kielezo Cha Fasili by Shaaban Robert

KShs790.00
Katika kazi hii muhimu, Shaaban Robert anatoa miongozo kwa waandishi na washairi kuhusu utunzi wa mashairi, na pia kuhusu misingi na sifa za uandishi mzuri.

Mwongozo wa BEMBEA ya Maisha

KShs400.00 KShs350.00
Ni mwongozo wa kumsaidia mwanafunzi kuchambua Tamthilia ya BEMBEA ya Maisha kwa mujibu wa wahusika, sifa za wahusika, fani, dhamira, msuko na maudhui

NITAAMINI NIONAPO

KShs1,000.00 KShs900.00
Wema hukuza mema, mikosi na tufani za maisha zilimnyang'anya Stella wazazi. Akajikutamikonono mwa wenyeji walalahoi. Nap wakamuani. Hatua kwa hatua alipanda ngazi kwa usaidizi wa kijana Ombaomba. Akawa awika ndani na nje ya nchi kupitia talanta yake.

SUMU YA PANYA by Isaac Wambedha

KShs1,000.00 KShs900.00
Riwaya hii inasimulia vituko vya Biandis katika Jimbo la Aboke, aliyedai kuwa ni walii wa Mungu. Hulka zake lakini zilikiuka kaida za uwalii wa Mungu. Wazee wakabaki kuduwaa.

Chochoro Za Madaraka(Alleys of Power)...

KShs1,200.00
Jasusi na Mwanadiplomasia nguli Joseph Kaduma ama Joe kama alivyozoeleka kuitwa akishirikiana na wenzake wanafanikiwa kumtoa madarakani Rais Sylvester Costa na hivyo kumweka mmoja wa mwenzao kuwa Rais wa Stanza, Habib Chamchua. Lakini hali inageuka kuwa tofauti na walivyokusudia, Korea Kaskazini nchi waliyoitumia kuwasaidia kutimiza azma ile ya kumtoa Rais Costa madarakani wanakuja na matakwa mazito yasiyotekelezeka.Joe na Rais Habib wanakuwa katika wakati mgumu wa ama kutekeleza takwa lile ama kuingia uadui na Korea Kaskazini. Wanaamua kutokutekeleza na hivyo kuingia kwenye msuguano mzito na Korea Kaskazini. Hali inakuwa ya sintofahamu kubwa hadi kupelekea Rais Habib kupotea Ikulu. Ni mtafutano usio wa kawaida.

Sauti Za Washairi by Matata Hassan

KShs700.00 KShs550.00
Diwani hii ni kamilifu katika kukuza lugha ya mwanafunzi pamoja na kumtayarisha katika mtihani wake wa kitaifa. Ndani ya diwani hii, mwanafunzi atakumbana na maelekezo kamili kama vile Sifa mbali mbali za mashairi, bahari, jinsi ya kuutumia Uhuru wa mshairi, Pasona/nafsi neni, lugha ya nadhari na mengine mengi. Fauka ya hayo, mwanafunzi pia atakumbana na maswali na majibu ya mtihani wa kidato cha nne yatakayomsaidia katika kujiweka tayari na mtihani huo. Kwa kifupi, diwani hii ni chombo tosha kinachostahili kuabiriwa sio na mwanafunzi tu bali hata mwalimu anayepania kuwatayarisha wanafunzi vilivyo.

Kambi Ya Shetani by Edmond Ongeri

KShs450.00 KShs400.00
Kambi Ya Shetani ni Tamthilia inayozungumzia uozo katika jamii.

Kudra na Kevin Oyugi

KShs769.00 KShs649.00
Riwaya hii ya Kudra ni ya aina yake. Ni riwaya ambayo imeyamulika masuala ya kisasa na yanayoiathiri jamii kwa njia hasi ama chanya. Mhusika Kudra anajipata akitopea katika ukwasi wa aina yake licha ya kuzaliwa katika jamii ya ukata hohehahe. Hizi zinakuwa ni kudra za Mwenyezi Mungu au majaaliwa kama waambavyo wengine. Mbali na haya majaaliwa yake, anafikwa na mkosi pale ambapo rafiki yake wa chanda na pete Jane anafia katika chumba chake. Hii ni baada ya wao kulewa chopi na kusindikizwa kiamboni kwa Kudra na Bwana Majuto usiku uliotangulia. Je, haya ni majaaliwa pia? Kakaye Kudra, Oscar Mpimbi naye katika umasikini wake anafanikiwa kuchumbiana na Daktari Agnes aliyekuwa akimtibu mamaye kabla ya kuaga dunia. Oscar anampenda Agnes licha ya kuogopa kumjuvya hali ya hisia zake. Kwa upande mwingine, Agnes naye anampenda Oscar na kuamua kumfahamisha. Je, hii ni kudra ya Rabana pia? Utamu wa riwaya hii hauishii tu kuisoma kwa burudani ila pia kujifunza masuala ibuka na ainati katika jamii. Ni riwaya ya kizazi cha leo na uleo ndani mwake! Jipatie nakala ujifahamishe zaidi!

Walanyama na Mashairi Mengine by Ken ...

KShs800.00 KShs650.00
WALANYAMA ni diwani la mashairi yanayoonyesha taswira ya jamii ya sasa. Jamii ambayo imetawaliwa na dhulma, unyanyasaji, unafiki na jinsi mapenzi yamekosa maana kwa kuyapuuza maswala ya jadi. WALANYAMA ni nyenzo ya bahari mbalimbali za ushairi zilizoshughulikiwa kwa ukamilifu kwa manufaa ya jamii yote ya ulimwengu.