Showing 1–20 of 23 results

Mtumwa hadi Siti Binti Saad by Emmanu...

KShs690.00
Historia ya maisha ya Siti Binti Saad kama yalivyosawiriwa na Shaaban Robert na Nasra Mohamed Hilal, na sasa, katika tamthiliya hii ya kihistoria, itamfunulia msomaji wasifu na safari ya maisha ya mwanamama huyu. Katika historia ya safari ya Siti Bint Saad, msomaji atajifunza:
Kwamba, ushindi maishani unawezekana hata kama umetoka katika familia maskini kiasi gani.
Kwamba, ili kuwa nyota katika fani au karama yako, uvivu hauna nafasi bali juhudi na kufanya kazi usiku na mchana.
Kwamba, katika safari yako ya kufikia kilele cha mafanikio utapambana na 'marafiki waliojaa gele, tadi, inda, fitina, majungu na vikwazo vya kila aina. Yote haya yalimpata Siti, ila alipambana hadi akaibuka kidedea.
Kwamba, fani na kipaji chako si kwa faida yako binafsi pekee, bali zaidi ni kwa jamii yako.
Na kweli, nyimbo za mwanaharakati huyu zililenga kuwatetea wanyonge ikiwa ni pamoja na kukemea ukandamizaji na udhalilishaji wa mwanamke. Alikemea upindishaji wa sheria uliofanywa na matajiri kupitia hongo; ikiwa ni pamoja na wizi uliofanywa na wafanyakazi wa serikali maofisini na viwandani.
Mwandishi ametunga tamthilia hii ya kihistoria ili kumuenzi mwanaharakati huyu aliyeishi kabla nchi nyingi za Afrika hazijapata uhuru.

Julius Nyerere Kizimbani by Emmanuel ...

KShs590.00
Tamthilia hii inahusu tukio la kweli la kihistoria lililotokea mwaka 1985.

Mwinyi na manyani ya adili by Emmanue...

KShs690.00
Tamthilia hii inazungumzia hali ya maisha nchini Tanzania kabla na wakati wa utawala wa rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi(Mhe).

Nguzo Mama by Penina Muhando

KShs590.00
Nguzo mama ni tamthiliya inayozungumzia changamoto zinazowakabili wanawake kwenye jamii ambazo zimekuwa minyororo inayowazuia kufikia kilele cha ukombozi wao.

Nyerere na Safari ya Kanaani by Emman...

KShs690.00
Msingi na dafina ya tamthilia hii ni historia na lengo kuu la Mwalimu Julius Nyerere na TANU kutaka kujenga uchumi wa ujamaa na kujitegema mintarafu mwongozo wa kitabu cha azimio la Arusha, 1987.

Kumng’oa Nduli na Emmanuel Mbogo

KShs590.00
Tamthiliya hii inaakisi awamu mbili za utawala wa Diktera Idi Amin nchini Uganda Awamu ya kwanza ni kuanzia mwaka 1971 alipomng'oa Milton Obote na kujitangaza Rais wa maisha wa nchi ya Uganda. Katika awamu hii, mwandishi anasawiri utawala wa kikatili, mateso, vifungo na hata mauaji ya raia wa madaraja yote katika jamii. Awamu ya pili, Oktoba, mwaka 1978, jeshi la Idi Amin lilivamia Mkoa wa Kagera, nchini Tanzania. Katika uvamizi huu, wanajeshi wa Uganda walimuua Hans Poppe, Mkuu wa Polisi na raia wengine wengi na kutangaza kuwa Mkoa wa Kagera ulikuwa sehemu ya Uganda. Shambulio hili linasababisha Mwalimu Julius Nyerere kutangaza vita dhidi ya Nduli kupitia ile hotuba maarufu, akisema: Wamanchi! Sasa tuna kazi maja ta! Кumpiga! Sahabu ya kampiga tunaya! Niya ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga tunayo! Mwandishi anaonesha kuwa, hatimaye, mwaka 1979 Nduli Idi Amin aling'olewa na wanajeshi wa JWT. Akakimbilia Libya, na kufariki dunia akiwa huko Saudi Arabia, tarehe 16/8/2003. Hii ni tamthiliya muhimu kwa kila mpenda amani, haki na maendeleo kote duniani.

Kaputula la Marx

KShs590.00
Kaputula la Marx ni tamthiliya pekee ya Euphrase kezilahabi.