Showing all 5 results

Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya ...

KShs960.00

Fani ya Fasihi Simulizi, kwa Gredi ya 10, 11 na 12 kimeandikwa kwa utaalamu mkubwa ili kufanikisha kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa fasihi simulizi katika kiwango hiki. Kitabu hiki kimeshughulikia kwa kina na kwa njia ya wazi na nyepesi tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika mtaala wa Gredi ya Kumi hadi Gredi ya Kumi na mbili.

Katika kitabu hiki, utapata:

  • Ufafanuzi wa kina wa dhana ya fasihi kwa jumla na hususan fasihi simulizi.
  • Uchanganuzi wa kina wa tanzu na vipera lengwa vya fasihi simulizi na mifano maridhawa.
  • Tungo za kuchangamsha, kusisimua na vilevile kurahisisha ujifunzaji.
  • Shughuli zenye kushirikisha kikamilifu katika ujifunzaji.
  • Tathmini endelevu za kumwezesha mwanafunzi kujitathmini na kutathminiwa na wenzake au na mwalimu.
  • Tathmini ya mwisho wa sura ili kumpa mwanafunzi picha ya jumla kuhusu kiwango chake cha ufahamu wa utanzu na kipera husika.
  • Mazoezi murua yanayochochea ujifunzaji huku yakipima ngazi zote za maarifa au utambuzi.
  • Majaribio ya Tathmini yenye mazoezi na maswali anuwai yatakayomwezesha mwanafunzi kupima umilisi wake.
  • Majibu kwa Majaribio ya Tathmini ili kumwelekeza mwanafunzi kubuni mikakati ya kujiboresha.

Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya ...

KShs916.00
Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya 7, 8 na 9 kimeandikwa kwa utaalamu mkubwa ili kufanikisha kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa fasihi simulizi katika kiwango hiki. Kitabu hiki kimeshughulikia kwa kina na kwa njia ya wazi na nyepesi tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika mtaala wa Gredi ya saba hadi Gredi ya Tisa. n nKatika kitabu hiki, utapata: n
    • n
    • Ufafanuzi wa kina wa dhana ya fasihi kwa jumla na hususan fasihi simulizi.
n
    • Uchanganuzi wa kina wa tanzu na vipera lengwa vya fasihi simulizi na mifano maridhawa.
n
    • Tunga za kuchanga, kusisimua na vilevile kurahisisha ujifunzaji.
n
    • Shughuli zenye kushirikisha kikamilifu katika ujifunzaji.
n
    • Tathmini endelevu za kumwezesha mwanafunzi kujitathmini na kutathminiwa na wenzake au na mwalimu.
n
    • Tathmini ya mwisho wa sura ili kumpa mwanafunzi picha ya jumla kuhusu kiwango chake cha ufahamu wa utanzu na kipera husika.
n
    • Mazoezi murua yanayochochea ujifunzaji huku yakipima ngazi zote za maarifa au utambuzi.
n
    • Tathmini tamati yenye mazoezi na maswali anuwai yatayomwezesha mwanafunzi kupima umilisi wake na kumtayarisha kwa Tathmini ya Mwisho wa Gredi ya Tisa- KJSEA.
n
    • Majibu kwa Tathmini tamati ili kumwelekeza mwanafunzi kubuni mikakati ya kujiboresha.
n nDkt. Assumpta K. Matei ni msomi mwenye tajriba pana katika masuala ya elimu, utafiti, ufundishaji na tathmini. Ana uzoefu mkubwa katika ufundishaji wa Isimu, Lugha na Fasihi ya Kiswahili nchini Kenya. Baadhi ya vitabu alivyoandika ni pamoja na: Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili na Zawadi ya Thamani (novela). Vilevile, amashirikiana na wengine kuandika vitabu kama vile: Jipe Moyo (Diwani ya Mashairi), Kamusi ya Watoto na Upeo wa Ufahamu na Ufupisho.

Fani ya Ushairi

KShs690.00
'Fani ya Ushairi kwa Shule za Upili' ni kitabu kilichofanywa utafiti wa kina kuondoa dhana ya ugumu. Kitabu kimeandikwa kwa utaalamu mkubwa wa kumfafanulia mwanafunzi utanzu wa ushairi. Kila kipengele cha ushain kimeelezwa kwa npa nyepesi na kwa undani zaidi kwa lengo la kurahisisha uelewekapo. n nMada zote za ushairi kwenye silabasi ya Kiswahili kwa Shule za Upili zimeshughulikiwa kwa kina na mifano anuwai kutolewa. Kila mfano umefafanuliwa kwa undani wa kumpa mwanafunzi mwangaza zaidi katika mada husika. n nMwishoni mwa kila sura kuna maswali yaliyotolewa. Maswali haya yatamwezesha mwanafunzi kupima uelewa wake katika mada alizosoma. Yanatahini stadi zote za ufumbuzi.

Fani ya Fasihi Simulizi kwa shule za ...

KShs825.00
'Fani ya Fasihi Simulizi' kwa Shule za Upili kimeandikwa kwa lengo la kumfafanulia mwanafunzi tanzu na vipera vya fasihi simulizi kwa njia angavu na nyepesi. nMahitaji yote ya silabasi ya shule za upili yameshughulikiwa kwa kina. nMada zimejadiliwa kwa lugha rahisi na mifano anuwai ya uchanganuzi kutolewa. nYapo maswali yaliyotolewa mwishoni mwa mada. Maswali haya yanatahini stadi zote za ufumbuzi. Mwishoni mwa kitabu kumetolewa majibu ya baadhi ya maswali ya mazoezi. n nAssumpta K Matei ni mwalimu mwenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili. Pia ameandika vitabu kadha vya kufunzia lugha na fasihi ya Kiswahili.

Fani ya Isimujamii kwa shule za Sekon...

KShs525.00
'Fani ya Isimujamii kwa Shule za Sekondari' ni kitabu kitokanacho na juhudi za makusudi za kuziba pengo la ukosefu wa vitabu kwenye ufundishaji wa somo la Isimujamii katika shule za sekondari. Kitabu hiki kimeandikwa na wataalamu wenye tajriba pana katika taaluma ya lugha na ufundishaji wake. Ni zao la utafiti wa kina na tathmini ya mahitaji ya wanafunzi na jamii. Upekee wa kitabu hiki unatokana na jinsi kinavyozingatia mahitaji ya walengwa. Kitabu kimekusanya mada na vipengele vyote vya Isimujamii vilivyomo katika silabasi mpya na kuvizamia kwa uketo. Aidha, maudhui yameshughulikiwa kwa namna inayosisimua na kuchochea hamu ya wanafunzi na walimu. Maelezo nayo yametolewa kwa utoshelevu na kwa njia sahali inayobainisha kwa uwazi dhana na hoja ili kurahisisha usomaji na uelewa. Mifano kemkemi inayokita katika mazingira na miktadha halisi inayofahamika imetolewa ili kukipa kitabu nguvu za kipekee. Kila sehemu ina maswali yenye lengo la kuzindua fikira za walengwa, kuwapa mazoezi na kuwapiga msasa. 'Fani ya Isimujamii kwa Shule za Sekondari' kimeandikwa ili kukidhi kikamilifu mahitaji ya silabasi mpya ya Kiswahili na kuwapa wanaokitumia umilisi katika matumizi ya lugha kwenye nyanja mbalimbali. Kwa hakika kitabu hiki ni wenzo tosha kwa mwanafunzi anayejiandaa kuukabili ipasavyo, na kwa kujiamini, Mtihani wa Kiswahili wa Kitaifa wa Kidato cha Nne.