swahili

Showing all 10 results

Adili na Nduguze by Shaaban Robert

KShs690.00
"Ingawa kitabu hiki hutaja habari za malaika na majini, na viumbe wa ajabu, lakini ni kwa sababu ya utunzi tu. Mambo hasa yaliyotiliwa mkazo ndani yake ni ardhi na mimea yake; machimbo na hazina zake; mifugo na mazao yake; biashara na faida yake; safari na manufaa yake; utajiri na braka yake; ahali na heshima zao; na ndugu na matendo yao. Mambo haya huhusu watu wengi kama si dunia nzima." - SHAABAN ROBERT
Maudhui mazito yaliyobebwa na hadithi hii ya kusisimua yamekifanya kitabu hiki kitumike tena na tena katika kufundisha Fasihi ya Kiswahili katika ngazi ya Elimu ya Sekondari. - MHARIRI.

Kusadikika by Shaaban Robert

KShs690.00
Kusadikika ni nchi ya kufikirika. Haipo kwenye ramani wala katika simulizi za kale, bali ndani ya fikra na maono ya mwanadamu. Imezungukwa na upepo na iko angani kana kwamba ni wingu linaloelea. Katika nchi hii ya ajabu, Karama, mtu jasiri na mwenye maono, anapinga mfumo wa haki usio wa haki. Kupitia hadithi hii ya kipekee, Shaaban Robert anatusafirisha kutoka sehemu moja hadi nyingine za Kusadikika kupitia safari ya wahusika sita waliotumwa kutafuta mifumo mbadala ya utawala.
Ingawa ni hadithi ya kubuni, maswali yanayoulizwa ndani ya Kusadikika kuhusu haki, uongozi na maadili bado ni ya msingi hadi leo.

Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsin...

KShs690.00
Maisha yangu na Baada ya Miaka Hamsini ni simulizi mbili za maisha ya Shaaban Robert katika maneno yake mwenyewe.
Simulizi ya kwanza inatuonyesha Shaaban Robert akiwa kijana mwenye nguvu na afya njema, mfanyakazi hodari na aliyejawa mshawasha wa kutenda mema. Baada ya miaka hamsini ni sehemu ya pili ya maisha yake, ambamo anazungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kunyimwa kwake bima ya afya kutokana na kutopita vipimo, ushiriki wake katika kupigania uhuru na vilivile mwamko wake na hata kujikita na kutopea katika fani ya uandishi pamoja na changamoto alizokutana nazo.
Shaaban Robert anapata madhila ya kufiwa na mke wake wa kwanza. Upweke unachukua nafasi katika maisha yake na kuwa rafiki na mgeni wake wa kila siku. Upweke na mavune ya ulezi vinampa changamoto kubwa maishani.
Ndoa yake ya pili nayo haidumu, kwani mke wa pili naye anafariki. Wazo lake la kuoa linasakamwa na kupigwa vijembe na washairi wa pande zote toka bara mpaka pwani.
Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini ni safari ndefu ya mshairi Shaaban Robert, safari inayopitia zama zote tatu za historia ya Tanganyika. Ameishi chini ya ukoloni wa Wajerumani, uangalizi wa ukoloni wa Waingereza na na vilevile ameshiriki na Mwalimu Julius Nyerere kupigania na hatimae kupata uhuru wa Tanganyika. Hii ni safari yenye misukosuko na hila nyingi lakini yenye fanaka lukuki.

Wasifu wa Siti Binti Saad by Shaaban ...

KShs590.00
Wasifu wa Siti Binti Saad kinaeleza maisha na safari ya Siti binti Saad, mwanamke wa kwanza kuimba Taarab jukwaani na kuwa Malkia wa kwanza wa muziki huo Afrika Mashariki.

Kielezo Cha Fasili by Shaaban Robert

KShs790.00
Katika kazi hii muhimu, Shaaban Robert anatoa miongozo kwa waandishi na washairi kuhusu utunzi wa mashairi, na pia kuhusu misingi na sifa za uandishi mzuri.

Kufikirika by Shaaban Robert

KShs790.00 KShs590.00
Kufikirika ni nchi ya kufikirika tu. Haipatikani kwenye ramani wala haiwezi kuandikwa. Imezungukwa na Bahari ya Kufaulu, Milima ya Jitihada, Nchi ya Anasa na Nchi ya Majaribu. Njia ya kwenda huko hukanyagwa kwa fikra badala ya nyayo. Katika nchi hii ya ajabu, tunafuatilia hadithi ya mfalme mwenye nguvu na mali tele, lakini anayekumbwa na huzuni ya kutopata mrithi. Anatoa amri isiyo ya kawaida: waganga wa aina zote kutoka pembe zote za nchi waje kusaidia kutibu utasa wake na wa Malkia.
Katika simulizi hii ya kubuni yenye mizizi ya falsafa, Shaaban Robert anatufanya tutafakari kuhusu uongozi, thamani ya maisha, elimu, na wajibu wa jamii kwa pamoja. Hadithi hii ya kina inaeleza namna taifa linaweza kuangamia au kustawi kulingana na maamuzi ya viongozi wake na uhusiano wao na elimu, fikra huru, na ustawi wa jamii.

Uchu: Harakati za Willy Gamba Book 7...

KShs890.00
“Umesikia George Foreman amerudi ulingoni na kutwaa ubingwa?” Chifu aliuliza. “Sikusikia tu, nimeona kwenye Televisheni,” Willy Gamba alijibu. “Basi nataka na wewe urudi ulingoni” Chifu alisema kwa kutabasamu huku akipaka mkate siagi. Baada ya kufunga ndoa na mpenzi wa maisha yake, Willy Gamba anakuwa mtu mpya asiyetaka kujihusisha tena na purukushani zinazoweza kuhatarisha maisha yake na familia yake. Maamuzi yake hayo yanakosa nguvu pale anapolazimika kuwatolea uvivu viongozi wetu wa Kiafrika ambao wametawaliwa na tamaa ya kubaki kwenye madaraka ili wajilimbikizie utajiri, huku Waafrika wakizidi kudidimia katika dimbwi la umaskini na migogoro ya kisiasa. Safari hii Willy Gamba anajikuta Rwanda, akitafuta ukweli wa vipi mamilioni ya wananchi waliuawa na wananchi wenzao huku Afrika na dunia wakiangalia bila kutoka msaada wowote. Uzito wa suala hili unampelekea Willy Gamba kupambana na usaliti na ujahili wa kimataifa ambao uko tayari kuendeleza utawala wa mabavu ili tu maslahi ya watu wachache wenye ubinafsi yaweze kulindwa.

Kikosi cha Kisasi: Harakati Za Willy ...

KShs890.00
Ni nani hasa anayewaua viongozi wa wapigania uhuru? Kwa nini wengi wa viongozi hawa wameuawa jijini Kinshasa kuliko mahali pengine popote Afrika? Ili kukomesha vitendo hivi vya kijahili, Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) inakata shauri kuwasaka wauwaji hawa na kuwafagilia mbali. Willy Gamba, mpelelezi maarufu wa Afrika, anachaguliwa kuongoza kikosi cha wapelelezi wa Kiafrika kuwasaka. Kinshasa, jiji linalosifika kwa starehe zake linageuka uwanja wa mapambano kati ya vijana wapiganaji shupavu wakiongozwa na Willy Gamba, na wapinga mapinduzi wakiongozwa na Kaburu Pierre Simonard. Willy pamoja na kikosi chake wanalivamia jiji la Kinshasa kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo. Ndipo patashika ambalo halijawahi kutokea barani Afrika linapoanza na kuliwasha moto jiji hili…

Kikomo: Harakati za Willy Gamba Book ...

KShs790.00
Haikuwa kazi yake kujishughulisha na makosa ya jinai. Hivyo alishangaa kidogo Chifu alipomwamuru afuatilie tatizo la upungufu wa almasi. Isingekuwa kwa sura aliyoonyesha, angeweza hata kumjibu kuwa apeleke malalamiko yake kwa Kamishna wa Polisi au ampe uhamisho kwenda huko kama alikuwa hamhitaji katika idara yake. Siku hiyo, Chifu alivaa sura ya kutisha na Willy Gamba hakuwa na la kufanya ila kukubali. Kulikuwa na ushahidi kwamba almasi zilizouzwa katika masoko ya nje zilikuwa chache sana kulinganisha na kiasi kilichokuwa kinachimbwa. Kwa nini iko hivyo!? hilo ndilo suala lililomsumbua sana Chifu. Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai imejitahidi bila mafanikio. Askari Polisi, Joel, amegusa chanzo cha uhalifu, akafa na uhalifu ukaendelea. Chifu anamtuma mpelelezi Jack Mbwile, naye maiti yake inaokotwa ikielea katika Ziwa Victoria. Sasa jambo limekuwa zito na hakuna jinsi, lazima Willy Gamba ahusike…

Kufa na Kupona: Harakati za Willy Gam...

KShs1,000.00 KShs790.00
Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka ofisi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia. Kutokana na ishara maalumu inasadikiwa kuwa majasusi hao wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli, Willy Gamba, anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote na kuwapokonya nyaraka hizo. Kazi hiyo lazima ifanyike haraka kabla hawajaziuza kwa adui. Muda unazidi kwenda na mapambano ya kuwasaka majasusi hao yanazidi kuwa makali na hakuna huruma. Pande zote zinapoteza watu muhimu. Wapelelezi, majasusi na raia wengine wasio na hatia wanauwawa. Wakati wote huo Willy Gamba anaendelea na upelelezi wake mgumu na ndipo anapokutana na mrembo Lina. Lakini mrembo huyu yuko upande gani? Na Lulu je? Je Chifu yupo sahihi anapomwonya Willy Gamba asimwamini mwanamke yeyote mrembo? Willy Gamba na wenzake wanabanwa vilivyo lakini hawana ruhusa ya kushindwa. Maisha ya wengi yanawategemea. Ni mapambano ya kufa na kupona, lakini wanawashindaje maadui wakali kama hawa?
delivery

QUICK DELIVERY

Swift dispatch

ONLINE PAYMENT

Multiple options

EXPERT SUPPORT

Help when you need it

WIDE VARIETY

Thousands of books

GLOBAL SHIPPING

Worldwide delivery

Shopping cart
Sign in

No account yet?

Shop
Filters
0 Wishlist
10 items Cart
My account