Showing all 8 results

Diwani Ya Mtokabara by Mwalimu M̵...

KShs1,000.00
Anayekitumia kitabu hiki atagundua kuwa Mashairi yote thelathini muundo wa tarbia ni mashairi bunilizi. Kumaanisha kuwa hayapatikani vitabu vingirne vilivyotangulia, Walakini, inafaa ijulikane ya kwamba utungo mzima ni ule wa kawaida kimuundo. Hali kadhalika mashairi katika kitabu hiki yamezoa maswali bunilizi na majibu yazo. Mtumiaji wa kitabu hiki atagundua ya kwamba mbali na kuwa mashairi ni ya kipekee, hata mazoezi na mazoezi na baadhi ya majawabu vilevile ni ya kipekee. Kwa kifupi, maswali na baadhi ya majibu hutayapata vitabuni vya hapo awali. Kulonga bayana, ni Kiswahili cha kawaida, maswali yaliyopatikana pamoja na majibu mengine hupatikana kwingineka.. Kitabu, Diwani Ya Mtokabara, ni kifupi mno. Mwalimu au/ na mwanafunzi wake ndio watakirefusha inavyotakikana na ni katika tamrini za mashairi yaya haya.

Andamano na Mohammed Ghassani

KShs850.00
Andamo ni diwani ya tungo za ushairi zilizoandikwa na Mohammed Ghassani kwa muongo mmoja kuanzia miaka ya mwanzoni ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Ni tungo zinazoogelea pamoja naye kwenye bahari ya uzoefu wa mwanzo wa ujana kuelezea hadithi yake ya maisha, mtazamo wake juu ya yale yaliyokuwa yakitokea mbele ya macho yake na ufahamu wake kwa ulimwengu. Aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Fasihi na Utamaduni ya Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Bwana Abbas Mdungi, wakati akikabidhi ripoti ya mswaada wa diwani hii mwezi Oktoba 2003, aliandika hivi:"Mshairi ameibuni kazi yake kwa ustadi mkubwa kama kwamba ni mweledi katika utunzi ilhali hii ndiyo kazi yake ya kwanza kabisa. Mitindo aliyotumia ni mingi na mizuri ambayo inatafautiana na wakati wengine kushabihiana....Kwenye lugha, ametumia lugha ya ushairi - nyoofu, nzuri na telezi... Maudhui, bila shaka, ameyatumia vizuri kuweza kuelimisha jamii akijikita kwenye masuala ya utamaduni, siasa na uchumi, ingawa utamaduni umekuwa sura kubwa zaidi.....Kwa kawaida, washairi wa Afrika huzikita dhamira zao katika migogoro ya kimapenzi, kindoa, kidini, kikazi, kinyonyaji, kidemokrasia, uongozi mbaya, umangimeza, njaa, umasikini na maradhi, naye kwa ujumla amefanikiwa sana katika hilo...." Kwa hivyo, ndani ya Andamo, sio tu muna mwangwi wa sauti ya kijana anayejaribu kuiwasilisha hadithi yake kwa hadhira kwa njia ya kishairi, lakini pia ishara ya kuibuka kwa kipaji cha aina yake kwenye uwanja wa fasihi ya Kiswahili.

Hidaya ya Penina Muhando 1

KShs1,150.00
Hidaya ya Penina Muhando ni mkusanyiko wa kazi mujarabu za mwandishi hodari wa tamthiliya, Profesa Penina Oniviel Muhando, ambaye ,kwa mchango wake adhimu katika lugha ya Kiswahili, hususan utanzu wa tamthiliya, anastihili kutambuliwa kama Mama wa Tamthiliya ya kiswahili.

Hidaya ya SHAABAN ROBERT 6

KShs1,150.00
Kina vitabu vitatu ambavyo ni kazi ya Shabaan Robert: Wasifu wa siti Binti Saad, Maisha yangu na baada ya miaka hamsini ( anasimulia maisha yake katika awamu mbili ,yaani kabla ya miaka hamsini na baada ya miaka hamsini) na Mwafrika aimba.

Hidaya ya SHAABAN ROBERT 5

KShs1,150.00
Kina vitabu vitatu ambavyo ni kazi ya Shabaan Robert: Pambo la lugha, Mashairi Ya Shaaban Robert na Tenzi za marudi mema na Omar Khayyam.

Hidaya ya SHAABAN ROBERT 1

KShs1,150.00
Kina vitabu vitatu ambavyo ni kazi ya Shabaan Robert: Ashiki kitabu hiki , Mapenzi bora na Insha na mashairi.