Showing 1–20 of 79 results

Njama:Harakati za Willy Gamba Book 4 ...

KShs890.00
Mpelelezi mashuhuri wa Afrika, Mtanzania, Willy Gamba, akiwa likizoni huko Afrika Magharibi, jijini Freetown, Sierra Leone, anatumiwa ujumbe wa haraka arudi upesi nchini kwani kumetokea hujuma kubwa. Kutokana na uzalendo wake hapotezi muda, hima anarejea nchini. Chifu wake anamweleza kuwa shehena kubwa ya silaha za kivita ambazo ni mali ya wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika, imeibiwa bandarini, katika mazingira ya kutatanisha. Habari hizi zinaleta utata mwingi, baadhi ya nchi zikisema ni njama za Makaburu, na nyingine zikisema ni njama za Tanzania. Katika kiza kinene kinachozunguka suala hili, serikali ya Tanzania inamtuma Willy kuwasaka. Hapo ndipo patashika zinaanza na jiji la Dar es Salaam linakumbwa katika wimbi la msukosuko wa uhaini, usaliti, na mauaji ya kikatili…

Siri ya Sarufi

KShs1,589.00 KShs1,463.00
Siri ya Sarufi ni Kitabu cha gredi ya 10, 11 na 12. Kimeangazia mada zote katika viwango hivi pamoja na tathmini zenye majibu baada ya kila mada teule. Siri ya Sarufi itakata kiu yako ya ufanisi.

DUA ZA USHINI – TIMOTHY O. SUMBA

KShs499.00 KShs399.00
Dua za Ushindi inafungua ukurasa wa maisha ya Mwenge, kijana anayekabiliana na changamoto za kila siku lakini anashikilia imani kama nguzo yake kuu. Kupitia simulizi iliyojaa matumaini, uthabiti na uhalisia, kitabu hiki kinaonesha jinsi dua zinavyoweza kubadilisha mwelekeo wa maisha—kutoka hali ya kawaida hadi ushindi wa kipekee. Ni kazi inayogusa nafsi, ikiwahamasisha wasomaji kuamini, kusimama imara, na kupigania hatima yao bila kukata tamaa. “Kazi ya kuhamasisha inayojenga imani na matumaini.”— Elizabeth “Simulizi yenye nguvu kuhusu ushindi wa ndani.” — Sifa “Inakufundisha kuona ushindi hata katikati ya changamoto.”—Joash

AFUENI – TIMOTHY O. SUMBA

KShs499.00 KShs399.00
Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, ambapo vijana wengi wanakabiliwa na shinikizo la maisha, Afuen​i inasimulia kwa undani safari ya Elifela—msichana anayesukumwa na msongo wa mawazo, kupoteza mwelekeo, na changamoto za kiuchumi. Kupitia simulizi iliyojaa hisia, uhalisia na mafunzo ya kina, msomaji anapelekwa kwenye safari ya kujitambua, kutafuta msaada, na hatimaye kupata mwanga katikati ya giza. Hiki si kitabu cha kusoma tu, bali ni mwongozo wa kufikiri, kuhimili, na kushinda. “Kazi ya kipekee inayogusa moyo na kuamsha akili.” — Anita “Simulizi halisi ya kizazi kinachopambana kimyakimya.”—Mohammed “Kitabu kinachokupa tumaini bila kupunguza uhalisia wa maisha.”—Janet

RAMANI YA KISWAHILI GREDI 10,11,12

KShs1,800.00 KShs1,500.00
Huu ni mwongozo madhubuti unaowaongoza wanafunzi wa Gredi ya 10,11,12 katika safari ya umahiri wa lugha chini ya mfumo wa CBE. Kitabu hiki kimeandikwa kwa umakini ili kusaidia wanafunzi kujenga stadi za mawasiliano ,kifikiri kwa kina na kujiamini katika matumizi ya lugha katika maisha halisi.

Diwani Ya Mtokabara by Mwalimu M̵...

KShs1,000.00
Anayekitumia kitabu hiki atagundua kuwa Mashairi yote thelathini muundo wa tarbia ni mashairi bunilizi. Kumaanisha kuwa hayapatikani vitabu vingirne vilivyotangulia, Walakini, inafaa ijulikane ya kwamba utungo mzima ni ule wa kawaida kimuundo. Hali kadhalika mashairi katika kitabu hiki yamezoa maswali bunilizi na majibu yazo. Mtumiaji wa kitabu hiki atagundua ya kwamba mbali na kuwa mashairi ni ya kipekee, hata mazoezi na mazoezi na baadhi ya majawabu vilevile ni ya kipekee. Kwa kifupi, maswali na baadhi ya majibu hutayapata vitabuni vya hapo awali. Kulonga bayana, ni Kiswahili cha kawaida, maswali yaliyopatikana pamoja na majibu mengine hupatikana kwingineka.. Kitabu, Diwani Ya Mtokabara, ni kifupi mno. Mwalimu au/ na mwanafunzi wake ndio watakirefusha inavyotakikana na ni katika tamrini za mashairi yaya haya.

English- Kiswahili Flashcards: Bible ...

KShs1,100.00
Improve your written and spoken Kiswahili with these interactive flashcards. These flashcards feature 37 of the most popular bible verses translated in English and Kiswahili, to help you improve your reading skills in either language. Read them out loud to perfect pronunciation, tone and confidence. The cards are designed to foster learning for people of all ages, either alone or in a group setting.

Watoto wa Maman’tilie by Emmanu...

KShs690.00
Katika riwaya hii, mwandishi  anathibitisha kuwa mama ni mtu wa muhimu sana. Inasimulia na kushadidia kuwa Maman'tilie ni nguzo na dereva wa familia yake yenye wasafiri watatu.

Dunia Hadaa by Hammie Rajab

KShs690.00
Ndoa ilioanza kwa tabasamu inageuka kuwa shubiri na kuzua sintofahamu. Je, ni mapenzi ya kweli au mtego uliovikwa sura ya ndoto?