Fiction and Non Fiction

Showing 81–100 of 2173 results

Masimulizi Kamilifu Ya Alfu Lela U Le...

KShs890.00
Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa hadithi maarufu duniani kote za Alfu Lela U Lela (au Siku Elfu Moja na Moja) zenye asili ya Arabuni na Uajemi. Masimulizi haya ya Alfu Lela U Lela yametafsiriwa kutoka matoleo ya Kiingereza na Kijerumani. Lugha hizi za Ulaya ndimo zilimotafsiriwa hadithi hizi kwa mara ya kwanza kutoka katika lugha za Kiajemi, Kiarabu na Kihindi.

Alfu Lela U Lela Book 1 by Hassan Ad...

KShs890.00
Hiki ni kitabu cha Kwanza katika mfululizo wa hadithi maarufu duniani kote za Alfu Lela U Lela (au Siku Elfu Moja na Moja) zenye asili ya Arabuni na Uajemi. Masimulizi haya ya Alfu Lela U Lela, yametafsiriwa kutoka matoleo ya Kiingereza na Kijerumani. Lugha hizi za Ulaya ndimo zilimotafsiriwa hadithi hizi kwa mara ya kwanza kutoka lugha za Kiajemi, Kiarabu na Kihindi. Tafsiri ya Kiingereza ilifanywa na Sir. Richard Burton, ambaye anafahamika huku kwetu kama mmoja wa wasafiri wa kwanza kutoka Ulaya kutembelea na ati “kuvumbua” sehemu zile walizofika. Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ilifanywa mwaka wa 1928 na katika kufanya hivyo, sehemu nyingi zilikatwa au ziliachwa makusudi bila kuzitafsiri kwa sababu wamisionari hawakutaka wasomi wa Kiswahili wasome baadhi ya sehemu kwa sababu zao wenyewe. Matoleo haya, kwa kifupi, ndiyo yenye hadithi kamilifu kwa uhakika; yaani mtiririko wa visa na maana halisi ya hadithi kama zilivyotungwa na kutafsiriwa na magwiji wa lugha hizo mbili zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Kiswahili kina bahati ya kumpata mfasiri, Hassan Adam, Mtanzania mwenye ujuzi wa lugha zote tatu zilizohusika katika kutayarisha tafsiri hizi. Bwana Hassan Adam ni mkufunzi wa miaka mingi katika Taasisi ya Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.

Barua Ndefu Kama Hii by Mariam Bâ

KShs690.00
Ramatoulaye, mwanamke Msenegali ameolewa na Modou, mtu mzito serikalini. Baada ya miaka mingi ya ndoa, Modou anaoa mke mwingine, msichana mdogo mwenye umri sawa na wa binti yake. Ramatoulaye anasahauliwa; pesa na mapenzi vinahamia kwa mke mdogo. Modou anakufa katika ajali ya gari. Nani atakayerithi mali za marehemu? Halafu kuna umati uliokuja kwenye kilio ambao “lazima ulishwe na upewe pesa kwa heshima ya marehemu”. Mariama Bâ, mwandishi wa riwaya hii, alikuwa wa kwanza kupewa tuzo ya NOMA mwaka 1980. Riwaya hii imetafsiriwa katika lugha 18 na umaarufu wake unazidi kukua. The original publication was in French, Une si longue lettre; and this is the Swahili translation from the English, translated by the late Professor Maganga. Une si longue lettre is a classic of the African canon, winning the first NOMA Award for Publishing in Africa in 1980, and translated into 18 other languages. About the author Mariama Bâ was a novelist, teacher and feminist, active from 1979 to 1981 in Senegal, West Africa. Bâ’s source of determination and commitment to feminism were stemmed from her background, her parent’s life and her schooling. Indeed, her contribution is of absolute importance in modern African studies since she was among the first to illustrate the disadvantaged position of women in African society. Bâ’s work focused on the grandmother, the mother, the sister, the daughter, the cousin and the friend, how they all deserve the title “mother of Africa”, and how important they are for the society.

Adili na Nduguze by Shaaban Robert

KShs690.00
"Ingawa kitabu hiki hutaja habari za malaika na majini, na viumbe wa ajabu, lakini ni kwa sababu ya utunzi tu. Mambo hasa yaliyotiliwa mkazo ndani yake ni ardhi na mimea yake; machimbo na hazina zake; mifugo na mazao yake; biashara na faida yake; safari na manufaa yake; utajiri na braka yake; ahali na heshima zao; na ndugu na matendo yao. Mambo haya huhusu watu wengi kama si dunia nzima." - SHAABAN ROBERT
Maudhui mazito yaliyobebwa na hadithi hii ya kusisimua yamekifanya kitabu hiki kitumike tena na tena katika kufundisha Fasihi ya Kiswahili katika ngazi ya Elimu ya Sekondari. - MHARIRI.

Kusadikika by Shaaban Robert

KShs690.00
Kusadikika ni nchi ya kufikirika. Haipo kwenye ramani wala katika simulizi za kale, bali ndani ya fikra na maono ya mwanadamu. Imezungukwa na upepo na iko angani kana kwamba ni wingu linaloelea. Katika nchi hii ya ajabu, Karama, mtu jasiri na mwenye maono, anapinga mfumo wa haki usio wa haki. Kupitia hadithi hii ya kipekee, Shaaban Robert anatusafirisha kutoka sehemu moja hadi nyingine za Kusadikika kupitia safari ya wahusika sita waliotumwa kutafuta mifumo mbadala ya utawala.
Ingawa ni hadithi ya kubuni, maswali yanayoulizwa ndani ya Kusadikika kuhusu haki, uongozi na maadili bado ni ya msingi hadi leo.

Kufikirika by Shaaban Robert

KShs790.00 KShs590.00
Kufikirika ni nchi ya kufikirika tu. Haipatikani kwenye ramani wala haiwezi kuandikwa. Imezungukwa na Bahari ya Kufaulu, Milima ya Jitihada, Nchi ya Anasa na Nchi ya Majaribu. Njia ya kwenda huko hukanyagwa kwa fikra badala ya nyayo. Katika nchi hii ya ajabu, tunafuatilia hadithi ya mfalme mwenye nguvu na mali tele, lakini anayekumbwa na huzuni ya kutopata mrithi. Anatoa amri isiyo ya kawaida: waganga wa aina zote kutoka pembe zote za nchi waje kusaidia kutibu utasa wake na wa Malkia.
Katika simulizi hii ya kubuni yenye mizizi ya falsafa, Shaaban Robert anatufanya tutafakari kuhusu uongozi, thamani ya maisha, elimu, na wajibu wa jamii kwa pamoja. Hadithi hii ya kina inaeleza namna taifa linaweza kuangamia au kustawi kulingana na maamuzi ya viongozi wake na uhusiano wao na elimu, fikra huru, na ustawi wa jamii.

Uchu: Harakati za Willy Gamba Book 7...

KShs890.00
“Umesikia George Foreman amerudi ulingoni na kutwaa ubingwa?” Chifu aliuliza. “Sikusikia tu, nimeona kwenye Televisheni,” Willy Gamba alijibu. “Basi nataka na wewe urudi ulingoni” Chifu alisema kwa kutabasamu huku akipaka mkate siagi. Baada ya kufunga ndoa na mpenzi wa maisha yake, Willy Gamba anakuwa mtu mpya asiyetaka kujihusisha tena na purukushani zinazoweza kuhatarisha maisha yake na familia yake. Maamuzi yake hayo yanakosa nguvu pale anapolazimika kuwatolea uvivu viongozi wetu wa Kiafrika ambao wametawaliwa na tamaa ya kubaki kwenye madaraka ili wajilimbikizie utajiri, huku Waafrika wakizidi kudidimia katika dimbwi la umaskini na migogoro ya kisiasa. Safari hii Willy Gamba anajikuta Rwanda, akitafuta ukweli wa vipi mamilioni ya wananchi waliuawa na wananchi wenzao huku Afrika na dunia wakiangalia bila kutoka msaada wowote. Uzito wa suala hili unampelekea Willy Gamba kupambana na usaliti na ujahili wa kimataifa ambao uko tayari kuendeleza utawala wa mabavu ili tu maslahi ya watu wachache wenye ubinafsi yaweze kulindwa.

Kikosi cha Kisasi: Harakati Za Willy ...

KShs890.00
Ni nani hasa anayewaua viongozi wa wapigania uhuru? Kwa nini wengi wa viongozi hawa wameuawa jijini Kinshasa kuliko mahali pengine popote Afrika? Ili kukomesha vitendo hivi vya kijahili, Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) inakata shauri kuwasaka wauwaji hawa na kuwafagilia mbali. Willy Gamba, mpelelezi maarufu wa Afrika, anachaguliwa kuongoza kikosi cha wapelelezi wa Kiafrika kuwasaka. Kinshasa, jiji linalosifika kwa starehe zake linageuka uwanja wa mapambano kati ya vijana wapiganaji shupavu wakiongozwa na Willy Gamba, na wapinga mapinduzi wakiongozwa na Kaburu Pierre Simonard. Willy pamoja na kikosi chake wanalivamia jiji la Kinshasa kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo. Ndipo patashika ambalo halijawahi kutokea barani Afrika linapoanza na kuliwasha moto jiji hili…

Kikomo: Harakati za Willy Gamba Book ...

KShs790.00
Haikuwa kazi yake kujishughulisha na makosa ya jinai. Hivyo alishangaa kidogo Chifu alipomwamuru afuatilie tatizo la upungufu wa almasi. Isingekuwa kwa sura aliyoonyesha, angeweza hata kumjibu kuwa apeleke malalamiko yake kwa Kamishna wa Polisi au ampe uhamisho kwenda huko kama alikuwa hamhitaji katika idara yake. Siku hiyo, Chifu alivaa sura ya kutisha na Willy Gamba hakuwa na la kufanya ila kukubali. Kulikuwa na ushahidi kwamba almasi zilizouzwa katika masoko ya nje zilikuwa chache sana kulinganisha na kiasi kilichokuwa kinachimbwa. Kwa nini iko hivyo!? hilo ndilo suala lililomsumbua sana Chifu. Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai imejitahidi bila mafanikio. Askari Polisi, Joel, amegusa chanzo cha uhalifu, akafa na uhalifu ukaendelea. Chifu anamtuma mpelelezi Jack Mbwile, naye maiti yake inaokotwa ikielea katika Ziwa Victoria. Sasa jambo limekuwa zito na hakuna jinsi, lazima Willy Gamba ahusike…

Kufa na Kupona: Harakati za Willy Gam...

KShs1,000.00 KShs790.00
Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka ofisi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia. Kutokana na ishara maalumu inasadikiwa kuwa majasusi hao wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli, Willy Gamba, anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote na kuwapokonya nyaraka hizo. Kazi hiyo lazima ifanyike haraka kabla hawajaziuza kwa adui. Muda unazidi kwenda na mapambano ya kuwasaka majasusi hao yanazidi kuwa makali na hakuna huruma. Pande zote zinapoteza watu muhimu. Wapelelezi, majasusi na raia wengine wasio na hatia wanauwawa. Wakati wote huo Willy Gamba anaendelea na upelelezi wake mgumu na ndipo anapokutana na mrembo Lina. Lakini mrembo huyu yuko upande gani? Na Lulu je? Je Chifu yupo sahihi anapomwonya Willy Gamba asimwamini mwanamke yeyote mrembo? Willy Gamba na wenzake wanabanwa vilivyo lakini hawana ruhusa ya kushindwa. Maisha ya wengi yanawategemea. Ni mapambano ya kufa na kupona, lakini wanawashindaje maadui wakali kama hawa?

Njama:Harakati za Willy Gamba Book 4 ...

KShs890.00
Mpelelezi mashuhuri wa Afrika, Mtanzania, Willy Gamba, akiwa likizoni huko Afrika Magharibi, jijini Freetown, Sierra Leone, anatumiwa ujumbe wa haraka arudi upesi nchini kwani kumetokea hujuma kubwa. Kutokana na uzalendo wake hapotezi muda, hima anarejea nchini. Chifu wake anamweleza kuwa shehena kubwa ya silaha za kivita ambazo ni mali ya wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika, imeibiwa bandarini, katika mazingira ya kutatanisha. Habari hizi zinaleta utata mwingi, baadhi ya nchi zikisema ni njama za Makaburu, na nyingine zikisema ni njama za Tanzania. Katika kiza kinene kinachozunguka suala hili, serikali ya Tanzania inamtuma Willy kuwasaka. Hapo ndipo patashika zinaanza na jiji la Dar es Salaam linakumbwa katika wimbi la msukosuko wa uhaini, usaliti, na mauaji ya kikatili…

Hofu: Harakati za Willy Gamba Book 4 ...

KShs1,000.00 KShs790.00
Mauaji ya kikatili yanafanyika karibu na mji wa Uitenhage nchini Afrika Kusini, siku ya kuwakumbuka wazalendo waliouawa mjini Sharpeville mwaka 1960. Makaburu wanajawa na hofu na wanatilia shaka kuwa ni njama za kikundi cha watu weusi kutaka kupindua serikali yao ya kibaguzi. Uongozi wa makaburu wa Afrika Kusini wakiongozwa na mkurugenzi wa shirika la ujasusi, kamanda wa jeshi la Kulfut na mkuu wa magaidi wasaliti wa UNITA wanakutana ili kukabili juhudi za ukombozi wa Afrika Kusini kwa kupanga wimbi la mauaji. Mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Kusini unafanyika Arusha, nchini Tanzania. Jambo hili linawatia hofu makaburu, hivyo basi, mikakati kabambe inafanywa na serikali yao ili kuusambaratisha mkutano huo. Umoja wa Wapigania Uhuru nao unaandaa kikundi makini kabisa ili kupambana nao na kuulinda mkutano huu muhimu. Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, hakosi panapokuwa na mapambano kati ya upande wenye haki, na ule wa dhuluma. Kwa kushirikiana na wapelelezi mahiri kutoka nchi za kusini mwa Afrika, wanakabiliana na makaburu hao na vikundi vya kigaidi vinavyoshirikiana nao. Hekaheka zinatokea Arusha, hofu inatanda kote! mwindaji awa mwindwaji…

Joy Beneath the Sun

KShs1,499.00 KShs1,000.00
Born into the harsh realities of rural Umuahia, Joy is the youngest of ten in a family struggling against poverty, superstition, and relentless societal pressures. While her siblings and relatives succumb to bitterness or misfortune, Joy’s unwavering faith, intelligence, and moral compass guide her through trials that would have crushed a lesser spirit. Refusing to compromise her integrity for love or wealth, she excels in school, earning a national scholarship to a prestigious university where she studies Computer Science. Yet, even as her academic brilliance opens doors, temptation and corruption loom—embodied in the predatory Mr. Kayode, whose promises of success come at the cost of morality. Through the unwavering support of Emeka, an honest and God-fearing agricultural engineer, Joy navigates the treacherous waters of ambition, romance, and spiritual trials. Her journey is punctuated by visions, biblical allusions, and dreams of a future that demands patience and courage. Alongside moments of suspense, betrayal, and heartbreak, Joy remains steadfast, learning the value of forgiveness, love, and resilience. From childhood hunger under mango trees to blistered hands working night shifts, from poisoned feasts to moral confrontations in the bustling streets of Lagos, Joy’s story is one of faith, love, and triumph. Ultimately, she rises to a First-Class honor in her degree, reconciles fractured relationships, and experiences a love redeemed, proving that those who sow in tears shall indeed reap in joy. “Joy Beneath the Sun” is a story of courage, morality, and the unyielding power of faith, illustrating how adversity, when met with resilience, leads to both personal and spiritual victory.

A Girl Cannot Go On Laughing All The ...

KShs700.00 KShs490.00
It's the city style as seen and lived by Nairobi's rising and trendy young men and women. There is vice and crime, violence and opulence, prostitution and hypocrisy. And in her face and love for life, sensational Edna is haunted by death, clings onto her carefree cassanova boyfriend Dave... It is Dave's turn, however, to learn that a girl cannot go on laughing all the time. The novel is as contemporary as it is courageous, as hiralious as it is harsh.
A Girl Cannot Go On Laughing All the Time is full of pathos, yet it is the one novel you may laugh to read.

The Gold Rush by Samuel Wachira

KShs1,000.00 KShs890.00
For Christopher Makumi, winning a scholarship to study in the United States was like getting the key to the doors of success, a chance of a lifetime, and a ticket to the world of riches. The truth is unveiled when the temptation of earning a quick fortune in the land of plenty leads him straight into the jaws of crime. Soon, he finds himself trapped between a ruthless crime lord, a bunch of dangerous killers and the law. The golden dream in the world of riches turns into a horrendous nightmare as the hunter becomes the hunted in a thrilling contest between the underworld and the law.
This is a dramatic story of an innocent young man who blindly falls into the trap of the lure of big money in a cliff-hanger which starts with false friendship. The friendship develops into double-cross, turns into a man-hunt and finally explodes into a blood chilling orgy of violence that leaves behind a series of assassinations.

JUSTICE IN THEIR HANDS

KShs1,399.00 KShs1,000.00
In a land suffocated by corruption, injustice, and failed leadership, the people’s cries for change are drowned out by the brutality of a system designed to oppress them. The government thrives on deception, its officials indulging in wealth stolen from citizens who can barely afford a meal. The police, once meant to serve and protect, have become executioners, their bullets silencing voices demanding accountability. Hospitals, meant to heal, become death traps where mysterious murders go unexplained. Schools and universities, the last hope for a better future, collapse under the weight of endless strikes and mismanagement. Amidst the chaos, a silent storm is brewing. Students, doctors, and ordinary citizens refuse to cower in fear. They take to the streets, their chants of justice growing louder with every fallen comrade. But the government responds with force, staining the roads with the blood of the innocent. When a patient is found murdered inside the most guarded hospital, and the security cameras conveniently fail to capture the culprit, it becomes clear—the system will protect its own at all costs. Yet, even in darkness, hope flickers. As fear gives way to rage, a resistance rises. Leaders emerge from unexpected places, uniting the oppressed in a final, desperate fight for justice. But with spies among them, betrayals looming, and a government willing to kill to maintain power, victory is uncertain. Will the people reclaim their nation, or will the corrupt system tighten its grip, silencing them forever? In Justice in Their Hands, the battle for freedom is not just about survival—it’s about rewriting history.

The Bloom That Refused To Wither by M...

KShs1,500.00
The Bloom That Refused to Wither is a moving story of pain, resilience, faith and hope. Through life's fiercest storms, Imani discovers that even the most battered soul can bloom again. Raw, heartfelt and deeply inspiring, this book will remind you that your scars do not define you—they can become the very place where healing begins.

Colour Her Great: African Heroines by...

KShs1,000.00 KShs800.00
Colour Her Great: African Heroines by Felgonah Oyuga

Life Sentence: Poetry, Musings and Pr...

KShs1,500.00 KShs1,300.00
Life Sentence: Poetry, Musings and Prose by Felgonah Oyuga

Ari ya Pasha by Gichimu Njeri

KShs500.00
Nyanya na mama wa mhusika mkuu, Pasha, wanashikilia kwamba msichana hana budi kupashwa tohara ndipo awe mke wa thamani siku za usoni. Wanapanga njama ya kumpasha tohara Pasha. Pasha anang’amua nia yao na kutoroka usiku. Anarudi mjini, anakoishi na wazazi wake. Soma hadithi upate maelezo zaidi.
delivery

QUICK DELIVERY

Swift dispatch

ONLINE PAYMENT

Multiple options

EXPERT SUPPORT

Help when you need it

WIDE VARIETY

Thousands of books

GLOBAL SHIPPING

Worldwide delivery

Shopping cart
Sign in

No account yet?

Shop
Filters
0 Wishlist
12 items Cart
My account