Challo Muusya ni mwandishi na mhakiki shupavu. Ana shahada za uzamili na uzamifu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta. Pia, ana shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Egerton. Ameandika tahakiki nyingi kwa shule za upili nchini Kenya na Uganda. Aidha, ameandika miswada kadha ya riwaya, hadithi fupi na hadithi za watoto. Baadhi ya hizi zipo katika mchakato wa uchapishaji. Kati ya vitabu vyake vilivyochapishwa ni pamoja na Magwiji wa Kiswahili: Kitabu cha Udurusu wa KCSE. Kitabu cha Sanaa ya Ushairi: Uchambuzi na Historia kitachapishwa hivi karibuni. Pia amechapisha makala nyingi za kitaaluma. Amefundisha katika shule kadha za upili nchini Kenya, ikiwepo Shule ya Upili ya Kaluva, kaunti ya Kitui. Amefudisha vilevile katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Kenya kama vile SEKU, Chuo Kikuu cha Machakos, CUEA na KAGEU.
QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery








































Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.