QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261




KShs600.00
Nuria Ranking: #88 in GovernanceNi Kitabu cha Kitaaluma, kilichoandikwa na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu ambaye ni Mwanasheria Kitaaluma, kuibua Mjadala wa kina barani Afrika wa Muktadha wa Kisheria juu ya dhana ya “USIRI NA UWAZI” wa Mikataba ya Uwekezaji ya Kimataifa (INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT-IGA) inayofanywa na Serikali za Nchi nyingi za Afrika ikiwemo Serikali ya Tanzania. Kitabu hiki Kimechambua kwa kina Sheria za Ndani (Tanzania-Case Study), Sheria za Kikanda (Afrika Nashariki na Afrika), Sheria za Kimataifa na Kuchambua Hukumu ya Mahakama juu ya Mgogoro wa Kisheria ulioibuka nchini Tanzania juu ya Uwekezaji wa Kimataifa baada ya Walalamikaji wazawa wa Tanzania kuamua kupinga Masharti ya Mkataba wa Uwekezaji Kimataifa (IGA).
Chimbuko kuu la kitabu hiki cha kihistoria, Kilichobatizwa jina; “UKUU, UHURU, USALAMA WA TANGANYIKA NA RASILIMALI ZAKE”, kilichohifadhi kumbukumbu Kitaifa na Kimataifa ya Raia wa Tanzania katika Kupigania Ukuu, Uhuru na Usalama wa Rasilimali za Tanganyika, Mwaka 2023/2024, ni kesi Mkakati iliyofunguliwa na Wanasheria Vijana[1] Katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya dhidi ya Mkataba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Bandari Tanzania (IGA) uliosainiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania na Kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na Matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Sheria Mbali mbali za Tanzania[2] zinazolinda Ukuu, Uhuru na Rasilimali za Nchi na vile vile Kinyume na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kama itavyojadiliwa kwa kina Katika Kitabu hiki.
Licha ya Mapungufu Makubwa ya Rais wa awamu ya tano, hayati, John Pombe Magufuli, kwenye Masuala ya Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria, Kitabu hiki kimemuelezea kwa kina, Hayati John Pombe Magufuli kama Rais kinara, Shujaa na Mfano wa kuigwa barani Afrika Katika Kuongoza Taifa la Tanzania lenye uwezo wa Kulinda Rasilimali zake kwa Utunzi wa Sheria za Kizalendo za ulinzi wa Rasilimali za Nchi na kulinda vile vile Ukuu, Uhuru, Usalama wa Tanzania na Rasilimali zake.
Kitabu hiki Kimefanya Uchambuzi wa Kina wa Maamuzi ya Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya nchini Tanzania, Maoni ya Wanazuoni, Vyama Vya Siasa, Taasisi zisizo za kiserikali na za kiserikali, Viongozi wa Kisiasa, Viongozi wa dini na taasisi za dini, Wanaharakati na Wadau mbalimbali Juu ya Mtizamo wao katika Masharti ya Mkataba wa Uwekejai baina ya Tanzania na Kampuni ya DP-Wold kutoka Dubai na Kutoa Mapendekezo ya kitaalamu kwa VIONGOZI WA TANZANIA, AFRIKA MASHARIKI NA AFRIKA kwa Ujumla wake.
Nchi Nyingi za Afrika ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi husika, zina utajiri mwingi wa Rasilimali lakini Mataifa ya Kigeni yamekuwa Wanufaika wakubwa wa Rasilimali husika kupitia Mikataba ya Kimataifa ya kinyonyaji ambayo Serikali za Nchi Nyingi za Afrika zinaingia na Mataifa husika na kuacha Umasikini Mkubwa kwa Wazawa na ufukara Mkubwa kwa wananchi huku kikundi cha Wachache ambao ni Watawala kunufaika na kuacha Bara la Afrika kutotimiza ndoto zake za Kujitegemea Kiuchumi na Kijeshi bali kubaki kuwa Vibaraka wa Mataifa ya Magharibi.
Kwa Ujumla wake, Kitabu hiki kimejadili ajenda hii ya “USIRI NA UWAZI WA MIKATABA YA KIMATAIFA” kama sehemu ya Kuchagiza Umajumui wa Afrika (Pan Africanism) na kuendeleza Maono ya Muda Mrefu ya Waasisi wa Umoja wa Afrika, pamoja na Wanaharakati mbalimbali wa Bara la Afrika katika kujitegemea Mathalani, Hayati Muamari Gadaffi, Julius Kambarage Nyerere, Nelson Mandela, Robert Mugabe, Nkwame Nkurumah, Jomo Kenyatta, Thomas Sankara, Martin Luther king, Che Geuvara na Wengine wengi.
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.