Zuka, Kazamoyo na wenzao wanacheza mchezo wa kamari chini ya shina la mkunazi, pesa zikiwa vizibo vya soda. Hapo shinani, mzee mwenye mkunazi ameyapanga mafungu ya kunazi ili ayatakaye, ayanunue. Kwa kuwa ilikuwa desturi yake kusinzia kila adhuhuri, yule mwenye mkunazi huwa anawachukulia hawa vijana kama walinzi wake; naye huwalipa kwa kuwapa kunazi. Hakuwa na uhakika ya kwamba, aliyepoteza pesa zake ilimbidi kulipa madeni yake kwa kunazi. Vijana hawa walifanya hivyo wakati wa adhuhuri. Ni kwa kuja kwake Jali, na kuonja kunazi moja, ndiko kusababishako vurumai liishalo tu kwa hawa vijana kupata fursa ya kusoma karatasi zilizorushwa matagaani. Ni baada ya kuzimaliza ndipo wanapogundua kwamba wamekuwa wakisoma hadithi iitwayo mafuta.
QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery















































Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.