Profesa K.ithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo K.ikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. Amewahi kufundisha katika Chuo K.ikuu cha Jimbo la Virginia (Virginia State University) Marekani, Chuo Kikuu cha Warsaw (University of Warsaw), Upolandi; na Chuo K.ikuu cha Masomo ya Kigeni cha Hankuk (Hankuk University of Foreign Studies), Korea Kusini. Mbali na kufundisha na kufanya utafiti, anajishughulisha na uandishi wa mashairi na tamthilia. Tamthilia yake maarufu iitwayo Kifo Kisimani ilikuwa kitabu cha lazima katika mtihani wa Kidato cha Nne nchini Kenya kuanzia mwaka wa 2006 hadi mwaka wa 2012. Tamthilia yake nyingine iitwayo Natala ilikuwa kitabu cha kutahiniwa katika vyuo vya walimu, pia nchini Kenya, kuanzia mwaka wa 2005 hadi mwaka 2016. Amewahi kukariri mashairi yake katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na nchini Kenya, Tanzania, Iran, Marekani, US Virgin Islands, United Arab Emirates, Upolandi, Ujerumani na Italia.
QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery























Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.