Kicheko cha Dhiki
Kuhusu Kitabu
Tamthilia ya Kicheko cha Dhiki inachora taswira kamili ya mataifa mengi ya Kiafrika.
Wananchi wa taifa la Sinzia wanashuhudia kuzorota kwa uongozi wa Mtemi Zedekaya. Fursa mpya ya kuchagua Mtemi mpya imebakia mikononi mwa wananchi hao. Je, vijana watapata nafasi ya kuongoza Sinzia? Je, Mtemi Zedekaya atabakia kuwa kiongozi wa Sinzia? Je, viongozi waliounga mkono Mtemi Zedekaya watampenda tena?
Tamthilia hii imemulika hulka ya viongozi waliochaguliwa debeni, asasi ya ndoa, nafasi ya vijana na kina mama katika jamii,na idara ya usalama kwa jumla. Suala la dini, ajira na ndoa limepigwa msasa. Mwandishi ana imani kuwa utagundua maudhui mengine, upate kuelimika ,na kuburudika.
Kuhusu Mwandishi
Kelvin Munene ni mtafiti na mwandishi wa fasihi. Ni mwandishi wa anthologia ya hadithi fupi iitwayo ‘Mitego ya Kisasa na Hadithi Nyingine’. Aidha, amejumuishwa katika mkusanyiko wa hadithi fupi unaoitwa “Simu ya Ajabu na Hadithi Nyingine ” ambapo hadithi yake ‘Chozi la Huba’ imehusika. Pia, ameandika riwaya ya “The Golden Jewels ” na tamthilia ya “The Fortnight Wizard”. Kwa sasa ni Naibu Mwenyekiti wa “Writers Guild ” katika Chuo Kikuu cha Chuka. Aidha ni mwanachama wa CHAKICHU ( Chama cha Kiswahili Chuka), Knowledge Ambassadors – Chuka na CHAWAKAMA- KENYA.



































Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.