Nasonga ni riwaya yenye mtazamo wa kina katika suala la ulezi wa mzazi mmoja na changamoto zake. Hadithi hii inamhsu Songa, mtoto wa kiume ambaye analazimika kupambana na hali ngumu ya maisha ili kufikia ufanisi ilivyo ada ya mja mwenye maono. Mamake Songa anatorokea jijini akikwepa ukeketaji na ndoa ya mapema na Lazima akiwa na tumaini la maisha bora. Hata hivyo, anatungwa mimba na mwanaume anayemdhania kuwa mwokozi. Bwana huyu anatoweka na kumwacha hoi, hana bee wala tee kummkuza mwanao katika mazingira ya chokoraa. Songa anapokuwa mtu mzima, ananusurika kumwoa dadake katika uvumbuzi unaopelekea kubadili maisha. Kupitia Nasonga, jinge na mwandishi Douglas Ogutu Vema anapolizamia jambo hili anapomulika kwa uwazi ukweli bayana wa matatizo katika familia pamoja na kuhimiza bidii katika jamii.