Fedha ni mtumishi mzuri lakini bwana mbaya. Zinapopewa nafasi ya kututawala, hutupotosha; lakini tunapozitawala kwa hekima, hutufungulia milango ya mafanikio na maendeleo. Hivyo basi, hata kama ulianguka jana, bado unaweza kusimama leo. Hata kama ulipoteza mengi, bado unaweza kujenga upya. Maadamu una pumzi, una nafasi ya kuanza tena.
Ni riwaya inayosimulia maisha ya mwandishi kutoka utotoni hadi utu uzima. Safari yake ya pandashuka maishani.
" Unaweza kusahau ladha nzuri ya Samaki uliyewahi kumla, ila huwezi kusahau MFUPA uliowahi kukuchoma kwenye fizi"